
Wakizungumza na Zanzibar24 huko katika Shamba la kuzalisha mimea ya
kilimo, Sheha wa shehia ya kilindi Ali Omar Mussa na mkulima Maryam
Hamad
wamesema mbali na kupokea mafunzo ya kilimo kupitia Mradi wa kaya
masikini TASAF lakini wanahitaji mafunzo zaidi ili waweze kuzalisha
mazao yenye kiwango.
Aidha wamesema uwepo wa mradi wa TASAF umewawezesha kujikwamua
kiuchumi na kuweza kutumia njia za asili katika kilimo bila ya kutegemea
mvua pamoja na kuwa na ujuzi wa kutengeneza mbolea ambayo ni salama kwa
watumiaji wa mazao yanayozalishwa.
Kwa upande wake Muwezeshaji wa Vikundi vya mbogamboga na matunda
kutoka TASAF Fatma Mwinyiwesa Idarusi amewambia wanakijiji hao kuzidi
kuitumia ipasavyo elimu wanazopewa katika kilimo ili kuweza kulinda afya
zao pamoja na kujiendeleza kiuchumi .

chanzo: Zanzibar24.
Comments