Shirika hilo, Proactiva Open Arms, limesema maafisa wake walipata
miili mitano ikielea karibu na boti mbili zilizokuwa zimezama, na ambazo
zina uwezo wa kubeba zaidi ya watu 100 kila moja.
Afisa wa
shirika hilo Laura Lanuza amesema miili ya watu hao watano
waliyofanikiwa kuitoa baharini inaonesha walikuwa wanaume wa umri mdogo.
Msemaji wa kikosi cha majini cha Italia, ambacho huratibu shughuli za uokoaji, amethibitisha vifo vya watano hao.
Hata
hivyo, amesema hawawezi kuthibitisha makadirio idadi ya waliofariki,
kama yalivyotolewa na Proactiva kwa kuwa hawakupokea vilio vyovyote vya
watu wakiomba msaada.
Bi Lanuza hata hivyo amesema wahamiaji 240 huenda walifariki kwani boti mara nyingi hujazwa watu kupita kiasi na walanguzi.
Shirika la kimataifa la uhamiaji (IOM) linasema zaidi ya wahamiaji 20,000 wamefika Italia mwaka huu kufikia sasa.
Watu 559 wanaaminika kufariki au kutoweka wakiwa safari kuelekea Ulaya kupitia eneo hilo.
Miezi mitatu ya kwanza ya mwaka 2016, kulikuwa na wahamiaji 19,000 waliowasili Italia na vifo 350.
chanzo:Bbc.
Comments