
Amesema kuwa kuna baadhi ya watu wanaonekana kuwa na mitazamo tofauti
kwake, akisema kuwa watu hao wameanza kuingia wasi wasi wa kuona kama
hatua hiyo inaweza kumfanya kuvunjika moyo katika kuunga mkoni jitihada
za chama hicho na kuamua kung’atuka ili kukwepa aibu kwa baadhi ya
wanachama.
Amesema suala hilo halina nafasi kwa
upande wake hata kidogo, akidai kuwa kuondolewa nafasi hiyo ni sehemu ya
uimarishaji wa chama hicho.
Aidha ameongeza kuwa, mabadiliko hayo ameyapokea kwa mikono miwili na
wala hana chuki na Mwenyekiti wa Chama hicho John Magufuli ambaye ni
msimamizi wa shughuli zote.
Hata hivyo amesema kuwa pamoja na kuizoea nafasi hiyo lakini bado
hajaathirika katika utendaji wake wa majukumu katika chama hicho na
kuahidi kuendelea kufanya kazi kwa bidii kwa ajili ya kukisaidia chama
chake.
Hata hivyo amesema ataendelea kutoa ushirikiano wake ndani ya chama
hicho ili waweze kupiga hatua zaidi za kukiimarisha chama chao.
chanzo: zanzibar24.
Comments