
Naibu Mkurugenzi wa Kampuni hiyo Kanda ya Kusini Mashariki ya Afrika
Bwana Kang Kai alisema hayo wakati Ujumbe wa Viongozi Sita wa Kampuni hiyo kutoka Nchini China na Mjini Dar es salaam ulipofanya mazungumzo na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Vuga Mjini Zanzibar.
Bwana Kang Kai alisema Kampuni ya CEICE imeamua kuwekeza miradi yao Zanzibar kwa lengo la kuunga mkono mpango Mkuu wa Serikali ya Jamuhuri ya Watu wa China wa kuelekeza nguvu zake za Uchumi katika kusaidia Maendeleo ya Bara la Afrika (China – Africa)
Alisema kutokana na ongezeko kubwa la vyuo Vikuu Bara la Afrika hivi sasa linazalisha wasomi wengi ndani ya vyuo hivyo kundi ambalo linaweza kutumia taaluma yao kupitia ushirikiano na Miradi inayotekelezwa na Kampuni ya CEICE.
Bwana Kang Kai alisema Kampuni ya CEICE imepiga hatua kubwa katika uzalishaji wa vifaa vya Kieletronik na kuviuza kwa Makapuni makubwa ya Kimataifa yakiwemo yale ya Sam sung na Sonny.

“ Mpango wetu wa kutaka kuwekeza Visiwani Zanzibar unalenga kutoa ajira pana katika miradi ya Viwanda pamoja na Umeme unaoambatana na mfumo wa kisasa wa ulinzi unaotumia umeme yaani Security System ”. Alisema Bwana Kang Kai.
Naye Mkurugenzi wa huduma za Vitega Uchumi na Maendeleo kutoka Mamlaka ya Uwekezaji Vitega Uchumi Zanzibar (ZIPA) Nd. Shariff Shariff aliueleza Ujumbe wa Viongozi wa Kampuni ya CEICE kwamba Serikali inahitaji Viwanda katika mpango wake wa kuelekea Nchi ya Viwanda.
Nd. Shariff alisema katika kuupa nguvu mpango huo Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imetenga eneo maalum ndani ya Ukanda wa Maeneo huru ya Uchumi yaliyopo Fumba kwa ajili ya Taasisi na Kampuni zinazohitaji kutaka kujenga viwanda vyao Zanzibar.

chanzo:zanzibar24.
Comments