Kwenye kanda hiyo fupi mwanamume huyo anasema, "Jina langu ni Kim Han-sol, kutoka Korea Kaskazini, moja wa familia ya Kim."
Anasema kuwa yuko na mama na dada yake lakini hakuna taarifa zaidi kuhusu ni wapi aliko. Haya ndiyo matamshi ya kwanza kutoka kwa familia ya Kim tangu kutokea mauaji hayo.
Babake aliuawa kwenye uwanja wa Kuala Lumpur tarehe 13 mwezi Februari, kwa kushambuliwa na kemikali ya VX.
Video hiyo ya dakika 40 inamuonyesha mwanamume ambaye anatambuliwa kuwa Kim Han-sol, akionyesha kile kinaonekana kuwa pasipoti ya Korea Kaskazini lakini yaliyomo kwenye pasipoti hiyo hayaonekani.
CHANZO;BBC
Comments