Urusi na China zimetumia kura ya turufu kuzuia jaribio la Umoja wa Mataifa la kutaka kuiwekea vikwazo serikali ya Syria.
Marekani, Uingereza na nchi nyengine katika Baraza la Usalama,
zilitaka kuiadhibu Damascus kwa tuhuma za kutumia silaha za sumu katika
maeneo ya waasi.
Ni mara ya saba sasa Urusi inatumia kura yake ya VETO kuikinga serikali ya Rais Assad na tuhuma za kimataifa.
Katika
hotuba yake iliyojawa hisia kabla ya kura, balozi wa Uingereza katika
Umoja wa Mataifa, Matthew Rycroft, alisimulia kifo cha mwathirika mmoja
ambae alipelekwa katika hospitali baada ya shambulio la gesi yenye sumu.
Hata
hivyo, kwa upande wake, balozi wa China katika Umoja wa Mataifa, Liu
Jieyi, ameliambia Baraza la Usalama kwamba bado hakuna vilelezo kwamba
serikali ya Syria imetumia silaha za kemikali.
Naye Rais Vladmir
Putin amesema vikwazo vitazuia jitihada za mazungumzo ya amani
yanayoendelea Geneva baina ya serikali na wapinzani wake.
Marekani
imesema Urusi na China zimekataa kuwajibisha vikosi ambavyo viliangusha
gesi za sumu na kusababisha vifo vya wanaume, wanawake na watoto.
chanzo:Bbc.
Comments