Mohammed Abdikheir, Mkurugenzi wa Masuala ya Dharura wa IOM amesema
kuwa, shambulio hilo dhidi ya boti ya wakimbizi karibu na Lango Bahari
la Bab al-Mandab katika mkoa wa Hodeida, pwani ya Yemen halikubaliki.
Amesema waliotekeleza shambulio hilo wangestahili kuangalia kwa makini
waliokuwa kwenye boti hiyo kabla ya kuchukua hatua yoyote.
Inaarifiwa kuwa, boti hiyo ilikuwa inatoka Yemen kuelekea Sudan
wakati iliposhambuliwa kwa kombora kutoka angani saa tisa usiku, kuamkia
Ijumaa ya jana.
Shirika la Kuhudumia Wakimbizi la Umoja wa Mataifa (UNHCR) pia
limelaani mauaji hayo ya wakimbizi na kuandika katika katika ukurasa
wake rasmi wa mtandao wa kijamii wa Twitter kuwa:
Tumeshangazwa na
shambulio hili, ni hujuma ya hivi punde dhidi raia wasio na hatia, na
mwendelezo wa matokeo hasi ya mgogoro wa Yemen. La kusikitisha zaidi ni
kuwa, wakimbizi hao ni halali ambao tunawatambua na wana vyeti halali
vya shirika hili."
Wakimbizi wa Kisomalia zaidi ya 42 wameuawa katika hujuma hiyo huku makumi ya wengine wakijeruhiwa.
chanzo;parstoday.
Comments