Bwana Guterres anasema malipo kwa ajili ya nchi ambazo hupeleka askari wa kulinda amani zishikiliwe iwapo uchunguzi hautafanyika kwa ufanisi.
Chini ya sheria ya Umoja wa Mataifa, nchi zinazochangia walinda Amani zinawajibika kuwawajibisha askari wake.
Bwana Guterres anasema fedha hiyo inaweza kwenda katika mfuko wa waathirika; amependekeza pia kuteua mawakili maalum kusaidia walioathirika.
Aliongeza kwa kusema kuwa bendera ya Umoja wa Mataifa haitatumika tena kufunika uovu unaofanywa na vikosi vya walinda usalama.
chanzo:BBC
Comments