Pia, watatoa ushahidi kuhusu tuhuma kwamba kulikuwa na ushirikiano na
mawasiliano kati ya Urusi na maafisa wa kampeni wa Rais Donald Trump.
Kadhalika, wataangazia tuhuma zilizotolewa na Bw Trump kwamba simu zake zilidukuliwa na mtangulizi wake Barack Obama.
Mkurugenzi mkuu wa Shirika la Uchunguzi wa Jinai la FBI James
Comey na mkuu wa Idara ya Taifa ya Usalama Mike Rogers watatoa ushahidi
katika kikao nadra sana cha wazi cha kamati ya bunge kuhusu ujasusi.
Bw Trump ametaja uchunguzi huo kuwa usio wa haki.
Urusi imekanusha tuhuma kwamba lijaribu kuingilia uchaguzi wa urais Marekani.
Januari,
mashirika ya ujasusi ya Marekani ,yalisema kuwa wadukuzi waliosaidiwa
na Urusi, walidukua akaunti za barua pepe za maafisa wa vyeo vya juu wa
chama cha Democrat na kufichua taarifa za aibu, ili kumsaidia bwana
Trump kumshinda Hillary Clinton.
Ripoti
ya mashirika ya CIA,FBI na NSA ilisema kuwa kiongozi wa Urusi Vladimir
Putin, aliamrisha kufanywa kampeni ya kushawishi uchaguzi huo.
Tangu wakati huo Trump amekumbwa na lawama kuwa timu yake ya kampeni ilikuwa na ushirikiano na maafisa wa Urusi.
Afisa wa Republican Davin Nunes, ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati
ya ujasusi pamoja na afisa wa Democrat Adam Schiff, wanaongoza uchunguzi
wa madai hayo.
Bwana Nunes siku ya Jumapili, alisema kuwa hajaona ushahidi wowote unaoonyesha kuwa Urusi iliingilia kampeni ya Trump.
Naye
mkurugenzi wa zamani wa idara ya kitaifa ya ujasusi James Clapper, naye
amesema kuwa hakuna ushahidi wowote kuonyesha kuwa Urusi ilihusika.
chanzo:Bbc.
Comments