Wanasanyasi waligundua kwamba tiba ya protini Hi1a ilifanya kazi ilipotumiwa katika panya wa maabara.
Wanasema
kuwa ilionyesha kwamba inaweza kuwa tiba nzuri katika siku za usoni ya
kiharusi lakini haijajaribiwa miongoni mwa binadamu.
Muungano
unaopigana dhidi ya ugonjwa wa kiharusi umesema kuwa utafiti huo bado
ungali katika awamu ya kwanza lakini unaunga mkono tiba yoyote inayoweza
kupunguza uharibifu unaofanywa na kiharusi.
Watafiti kutoka chuo
kikuu cha Queensland and Monash , walisafiri hadi kisiwa cha Fraser
nchini Australia kuwawinda na kuwasika buibui hatari wa taifa hilo.
Baadaye waliwachukua buibui hao katika maabara ili kuwatoa sumu hiyo.
Hatua hiyo ilishirikisha kuwabembeleza buibui hao kutoa sumu hiyo ambayo baadaye hutolea kwa kupitia bomba.
Walitoa protini hiyo na kutengeza kadhaa katika maabara.
Baadaye walimdunga panya protini hiyo ambapo iliweza kuzuia jeraha lolote katika ubongo.
chanzo:Bbc.
Comments