
Alisema hatua hiyo itafungua milango ya Uwekezaji kwa Taasisi na Makampuni ya Uwekezaji ya Jimbo la Kerala Nchini India kuanzisha miradi yao Zanzibar hasa ikizingatiwa kwamba Utamaduni pamoja na mazingira ya pande hizo mbili yanafanana.

Aliuomba Uongozi wa Jimbo la Kerala kupitia Shirikisho hilo la Viwanda Nchini India kuanzisha ushirikiano wa pamoja kati yake na Zanzibar hasa kwenye kilimo cha Viungo kwa vile Zanzibar tayari imeshabarikiwa kuwa na rasilmali kubwa ya Mazao yanayotokana na viungo.
Alisema Zanzibar bado inakabiliwa na ukosefu wa Utaalamu wa kutosha katika kuendesha miradi inayotokana na kilimo cha Viungo kiasi kwamba mapato yanayopatikana katika Kilimo hicho hayendi sambamba na nguvu zinazotumika.
Mapema Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi Nd. Juma Ali Juma aliueleza Ujumbe huo wa Shirikisho la Viwnada Nchini India kwamba Kilimo badokinategemewa kuwa muhimili wa Uchumi wa Zanzibar kilichoundiwa Sera katika kuona kinamkomboa Mwananchi hasa Mkulima.

Alifahamisha kwamba Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inaendelea na mipango ya kuimarisha Sekta ya Uvuvi katika bahari Kuu ambayo bado haijatumia ipasavyo ili iweze kutoa ajira nyingi zaidi kwa Wazalendo.
Nd. Juma alifafanua kwamba bidhaa zitakazotokana na mazao ya Baharini zinaweza kutoa mchango mkubwa wa chakula katika Sekta ya Utalii na kuipunguzia mzigo Serikali Kuu bidhaa hizo kuagizwa nje ya Nchi jambo ambalo huhitaji gharama kubwa ya Fedha.
Alisisitiza umuhimu wa kutumika kwa Teknolojia ya Kisasa katika uwekezaji unaoendelea kwa sasa utakaokidhi mahitaji halisi kwa vile Zanzibar ina eneo dogo la ardhi.
Kwa upande wake Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi ambae pia ni Waziri asiye na Wizara Maalum Zanzibar Dr. Sira Ubwa Mamboya alisema kundi kubwa la Wanawake na Vijana wanaomaliza masomo yao ya Sekondari bado wanahitaji kuungwa mkono.
Dr. Sira alisema kipato wanachokipata makundi hayo kwa sasa katika baadhi ya kazi wanazizifanya hakijaweza kukidhi mahitaji yao halisi ya kuendesha maisha yao ya kila siku.
Alisema uanzishwaji wa Viwanda Vidogo vidogo kwa mchango wa Taasisi na Makampuni ya ndani na nje ya Nchi ndio suluhu pekee itakayoliibuwa na kadhia hiyo kundi hilo ambalo ndilo kubwa katika Jamii.
Akitoa shukrani kwa niaba ya Ujumbe wa Shirikisho la Viwanda Nchini India {CII} Makamu Mwenyekiti wa Shirikisho hilo Bwana George Paul aliueleza Ujumbe wa Zanzibar kwamba Taasisi zilizo chini ya mwamvuli wa Shirikisho hilo zimepata shauku ya kuangalia namna zinavyoweza kuelekeza nguvu zao za Uwekezaji Visiwani Zanzibar.
chanzo:zanzibar24..
Comments