
Akitoa Mafunzo kwa waandishi wa habari Mwakilishi kutoka shirika la kimataifa linalosaidia watoto Save the Children
Ellen Otaru amesema hivi sasa waandishi wengi nchini pamoja na vyombo vya habari vimekuwa vikiandika habari mbalimbali zinazowahusu watoto ambapo hufanya udhalilishaji bila ya kujijua hivyo ipo haja ya kuzingatia maadili na kanuni za uwandishi hasa katika kutoa taarifa za udhalilishaji ili kuepuka nayeye kumdhalilisha mtoto.
Hata hivyo amesema ili kuepuka makosa hayo waandishi wanapaswa kuandika taarifa zisizo na ukinzani na kuepuka kutoa picha ambazo zinaharibu maadili na haki ya mtoto, kumpa uhuru mtoto wa kuongea pindi anapopata tatizo bila ya kutumia nguvu au hongo kwa watoto ili kutoa taarifa.

chanzo: Zanzibar24
Comments