Kadogosa aliyasema hayo alipozungumza na waandishi wa habari Dar es
Salaam na kufafanua kuwa kampuni hiyo itatoa ajira za moja kwa moja 200
kutoka kwa vijana wa vyuo vikuu nchini.
Alisema watu hao 200 miongoni mwao watakuwepo wahandisi, mafundi,
makenika na wataalamu wengine wanaohusiana na masuala hayo ya rasilimali
za reli.
Alisema wataalamu watakaotoka vyuo vikuu watakuwa wa kwanza kupata
mafunzo kabla ya kujiunga na Rahco. Pia alisema mbali na kutengeneza
ajira nchini ujenzi huo utatoa nafasi ya biashara kwa Watanzania.
“Hatua hii ya ujenzi wa reli itatengeneza ajira katika vituo vya
biashara ambayo itatoa nafasi kwa Watanzania hususan vijana kutengeneza
ajira mbalimbali,” alisema.
Katika hatua nyingine, Rahco imesisitiza kuwa waliovamia eneo la wazi la reli hiyo ni lazima waondoke haraka.
Akizungumzia malalamiko yaliyotolewa dhidi yao, alisema hatua ya
kuwaondoa wavamizi hao waliojenga pembezoni mwa reli hiyo ilifuata
sheria na miongozo.
“Waathirika wote walipewa notisi mwaka mmoja uliopita, na walikuwa
wakikumbushwa kubomoa nyumba zao,” alisema na kusisitiza kuwa wote
waliobomolewa ndani ya eneo hilo hawatapata fidia yoyote.
Alisema jumla ya nyumba 485 kutoa Dar es Salaam mpaka Pugu zilijengwa kimakosa katika eneo hilo la hifadhi ya reli.
chanzo:Habarileo.
Comments