Polisi mwandamizi kuhusu masuala ya ugaidi, Mark Rowley, pia amesema
wanaamini wanaweza kumtambulia mshambuliaji wa tukio hilo, lakini
hakutoa taarifa zaidi.
Raia watano wameuawa na wengine zaidi ya
arobaini kujeruhiwa na mtu aliyevurumiza gari sehemu ya kupitia watu
katika daraja la Westminister. Baadae kuingia katika viwanja vya bunge
ambapo alimchoka kisu polisi kabla ya kupigwa risasi.
Waziri mkuu
wa Uingereza, Theresa May, amesema tukio hilo ni la kusikitisha na
kutuma salamu zake za rambirambi ndugu wa wafiwa na kuwaombea
waliojeruhiwa.
chanzo:Bbc.
Comments