Katika tukio
hilo, askari mmoja amejeruhiwa kwa kuchomwa mkuki.
Tukio hilo
limetokea eneo la Relini katika Kijiji cha Kidomole, Kata ya Fukayosi.
Akizungumza na
Gazeti hili, Diwani wa Fukayosi, Ally Ally aliwataja vijana hao ambao ni ndugu,
kuwa ni Sainga Gheambalelega (21) na Rumay Gheambalelega (23).
Diwani huyo
amesema chanzo cha tukio hilo ni baada ya vijana hao kuwagomea askari kuswaga
ng’ombe hao wanaodaiwa kuibiwa kwenye zizi la mfugaji mwingine jina
linahifadhiwa kwa uslama.
Diwani huyo
amesema awali, polisi walipokea taarifa kutoka kwa mtu huyo aliyedai kaibiwa
mifugo yake na ameiona katika moja ya maboma ya wafugaji wenzake eneo la Relini.
“Ndipo polisi
wakaondoka kwenda kuiswaga wailete kwenye kituo chao wilayani Bagamoyo Mkoa wa
Pwani. Wakiwa njiani ndipo kundi la wafugaji liliwavamia na kuanzisha
vurugu,” amesema diwani huyo.
Kamanda wa
Polisi Mkoa wa Pwani, Boniventura Mushongi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo
na ameahidi kulitolea ufafanuzi kesho.
Chanzo:Mwananchi.
Comments