Abiria waliokuwa wakisafiri kwa ndege hiyo ya shirika la Uingereza,
walikuwa tayari wameingia ndani ya ndege hiyo wakati lilitolewa tangazo kuwa
ingechelewa.
Carly, ambaye alikuwa ndani ya ndege, alisema kuwa mhudumu
alitangaza, "walisema kitu kisicho cha kwaida kimetokea"
Kisha mhudumu huyo akasema wameambiwa ndege nyingine imepatikana
lakini abiria wangesubiri saa kadhaa ili kuanza safari.
Shirika la ndege la Uingereza lilisema; "Tunaelewa kuwa karibu
kila mtu anataka kusafiri nasi hadi San Francisco, lakini wakati huu kulikuwa
na mteja mdogo ambaye lazima tungemtoa.
"Kila
mmoja aliye na miguu miwili kwa sasa yuko safarini kuenda California, na
tunaomba radhi kwa kuchelewa."
chanzO:Bbc.
Comments