“Operesheni” ya viroba yapambamoto.

Mamlaka ya chakula na Dawa nchini -TFDA imeyafungia maduka kadhaa ya vinywaji katika Manispaa ya Temeke Jijini DSM kwa tuhuma za kukiuka  sheria, kanuni na taratibu za biashara hiyo.
Kufungwa kwa maduka hayo ni mwendelezo wa opersheni dhidi ya biashara ya vinywaji vinavyofungashwa katika vifungashio vya plastiki maarufu Viroba iliyoanzishwa na Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira.

Afisa afya wa Manispaa ya Temeke Rehema Sadick amesema miongoni mwa sababu zilizosababisha kufungwa kwa maduka hayo ni pamoja na maduka hayo kufanya biashara bila ya leseni kutoka TFDA, mamlaka ya mapato nchini TRA pamoja na kutozingatia kanuni za usafi.
Aidha amewataka wamiliki wa maduka hayo kufika katika mamlaka husika kwaajili ya kukamilisha kanuni na taratibu zote za uendeshaji wa biashara vinginevyo hatua zaidi zitachukuliwa ikiwa ni pamoja na kufikishwa mahakamani.
 chanzo:zanzibar24.

Comments