Taarifa zinasema nyoka huyo aliachwa kwenye ndege hiyo na abiria.
Alikuwa ameorodheshwa kama 'mnyama kipenzi' na abiria huyo katika safari nyingine iliyokuwa imefanywa na ndege hiyo.
Abiria
walifahamishwa kuhusu uwepo wa nyoka huyo rubani alipotangaza: "Jamaa,
tuna nyoka ndani ya ndege hii, lakini hatujafahamu yuko wapi hasa."
Nyoka
huyo wa futi tano hakuwa na sumu na alionekana mara ya kwanza kwenye
ndege na mvulana alikuwa amepanda na kusimama juu ya kiti.
Mvulana huyo alipomuona nyoka huyo, nyoka huyo alikuwa amelala na kufunikwa kiasi na begi.
Kwa mujibu wa mamake mvulana huyo, Anna McConnaughy, hakukutokea mtafaruku kwenye ndege hiyo.
Aliwekwa kwenye sehemu ya kuhifadhia taka kwenye ndege hadi ndege hiyo ilipowasili kwenye uwanja wa ndege Anchorage.
Wahudumu walifahamu kuhusu nyoka huyo mara ya kwanza abiria alipopiga
ripoti kwamba alikuwa amempoteza mnyama kipenzi wake akiwa safarini
kwenda Aniak katika jimbo la Alaska.
Alidokeza kwamba huenda mnyama huyo wake alikuwa kwenye ndege iliyokuwa safarini kurejea Anchorage.
chanzo:Bbc.
Comments