Msese amesema
iwapo majaribio hayo yatakamilika na meli hizo kuwa salama kwa ajili ya utoaji
wa huduma, wananchi wa pande hizo wataweza kuendesha shughuli zao kwa ufasaha.
Meli mbili za
mizigo zilizotengenezwa na Kampuni ya Songoro Marine zimeshushwa katika ziwa
hilo kwa ajili ya majaribio baada ya kukamilika kwa asilimia 95.
Meli hizo ni
kati ya tatu, ikiwamo ya abiria zinazojengwa kwa gharama ya Sh20 bilioni.
Msese amesema:
“Kila (meli) moja itakuwa na uwezo wa kubeba tani 1,000 za mizigo tofauti na
zilizopo zinabeba tani 720, hivyo kukamilika kwa meli hizi tutakuwa tumeleta
mapinduzi makubwa katika sekta ya usafirishaji wa majini badala ya kuendelea
kusafirisha mizigo kwa barabara”.
Mkurugenzi wa
kampuni hiyo, Saleh Songoro amesema kitakachofuata ni matengenezo madogo na
ukaguzi wa ubora kutoka Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini
(Sumatra).
chanzo:Mwananchi.
Comments