Ruhusa hiyo
imekuja ikiwa ni takriban mwezi mmoja tangu kupigwa marufuku uchimbaji
mchanga visiwani hapa.
Uchimbaji
unafanyika katika maeneo ya Mkoa wa Kaskazini Unguja, ambako viongozi wa
Serikali wameonekana kusimamia shughuli hiyo ili ifanyike kwa amani na utulivu.
Mkuu wa Wilaya
ya Kaskazini B, Issa Juma Ali amesema kikosi kazi cha usimamizi kitahakikisha
kazi hiyo inafanyika kwa mpangilio.
Baadhi ya
wamiliki wa magari ya mchanga, wamesema licha ya Serikali kufuta marufuku hiyo,
utaratibu uliowekwa siyo mzuri.
Mmiliki wa gari,
Juma Ahmada amesema utaratibu wa Serikali kusimamia uchimbaji ni mgumu hasa
katika suala la kupanga bei.
chanzo:Mwananchi
Comments