Mganga Mkuu wa
Kituo cha Afya Ikwiriri, Iddy Malinda amethibitisha mwili wa mwenyekiti huyo
kufikishwa kituoni hapo ukiwa na jeraha kubwa mgongoni lililotokana na risasi
aliyopigwa kifuani, upande wa moyo.
Mkuu wa Wilaya
ya Rufiji Juma Njwayo pia amethibitisha kutokea kwa mauaji hayo na kusema watu
wasiojulikana walifika nyumbani kwa mwenyekiti huyo kisha kumpiga risasi na
kutokomea kusikojulikana.
Habari zaidi
zinadai watu hao baada ya kutekeleza mauaji hayo hawakuchukua kitu chochote
kile.
chanzo:Mwananchi.
Comments