Mkurugenzi Mkuu wa REA, Gissima Nyamo-Hanga aliyasema hayo hivi
karibuni katika hafla ya uzinduzi wa mradi kabambe wa kusambaza umeme
vijijini awamu ya tatu katika Mkoa wa Singida uliofanyika kijijini
Mkwese wilayani Manyoni.
Nyamo-Hanga alimweleza mgeni rasmi katika uzinduzi wa mradi huo,
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo kuwa, ufanisi wa
kazi wa mkandarasi husika haukuwa mzuri hivyo kusababisha baadhi ya
vijiji ambavyo vilipangwa kupelekewa umeme katika REA II, kutofikiwa na
huduma hiyo.
“Tumechukua hatua za kinidhamu. Tumemsimamisha kazi na tutaleta
wakandarasi wapya ambao wataendelea na kazi ya kusambaza umeme pale
alipoishia,” alieleza mtendaji huyo wa REA.
Aidha, alitoa shukrani kwa serikali kwa ushirikiano na msaada ambao
imekuwa ikitoa, ulioiwezesha REA kuendelea na kazi ya kuwafikishia umeme
wananchi wa vijijini kwa mafanikio makubwa.
chanzo:Habarileo.
Comments