Mkuu wa magaidi wa ISIS asaidiwa na askari wa Marekani kutoroka Mosul.

Kinara wa kundi la kigaidi la ISIS au Daesh ameukimbia mji wa Mosul, Iraq kwa msaada wa askari wa Marekani katika eneo hilo.

Hayo yamedokezwa na Jawad Al Talibawi  kamanda wa Wapiganaji wa vikosi vya kujitolea vya wananchi Iraq maarufu kama Al-Hashd Al-Shaabi ambaye ameongeza kuwa, wanajeshi wa Marekani wamemsaidia Abubakar Al Baghdadi kutoroka na kujificha katika eneo la Al-Qayrawan. 

Amesema taarifa za kijasusi zinaonyesha kuwa kinara huyo wa ISIS yuko baina ya  Al-Qayrawan na eneo la Al Hadhr yapata kilomita 80 kusini mwa Mosul.
Siku ya Jumatano, Wizara ya Ulinzi ya Marekani, Pentagon ilisema kuna uwezekano kuwa Al Baghdadi ameondoka Mosul na kujificha katika maeneo ya jangwani nje ya mji huo. 
Siku chache zilizopita Al Baghdadi alitoa hotuba ya mwisho akikiri kushindwa kundi hilo nchini Iraq na akiwataka wafuasi wake kukimbilia maeneo ya milimani kwa usalama wao au kujiripua.
Magaidi wa ISIS wamekuwa wakiendesha kampeni ya mauaji ya kinyama nchini Iraq na Syria tokea mwaka 2014. 
 chanzo:parstoday.

Comments