Bwana Comey amesema kuwa amelitaka shirika la haki nchini humo
kukataa madai hayo kwamba Obama aliagiza uchunguzi wa simu za Donald
Trump wakati wa kampeni za uchaguzi uliokwisha.
Alikana madai hayo akisema kuwa yanayoonyesha FBI ilivunja sheria.
Hatua hiyo iliripotiwa na gazeti la the New York Times na kuthibitishwa na NBC.
Idara ya haki haikutoa taarifa ya mara moja kuhusu ombi la bwana Comey.
Vyombo
vya habari nchini Marekani viliwanukuu maafisa vikisema kuwa bwana
Comey anaamini hakukuwa na ushahidi kuthibitisha madai ya Trump.
Rais
huyo wa chama cha Republican ambaye anakabiliwa na uchunguzi mkali
kuhusu uingiliaji wa Urusi ili kuunga mkono uchaguzi wake hajatoa
ushahidi wowote kuunga mkono madai yake kwamba simu zake katika ofisi ya
Trump Tower zilidukuliwa.
chanzo:bbc.
Comments