
Hayo yameelezwa leo
huko katika ukumbi wa hoteli ya Misali sun set beach Wesha mkoa wa
kusini Pemba ambapo taasisi ya Milele Zanzibar Foundation iliwakutanisha
walimu wa somo la kiingereza kisiwani Pemba na wadau wengine wa sekta
ya elimu katika mkutano ulioambatana na mafunzo kwa lengo la
kuvitambulisha vitabu hivyo pamoja na kutoa mwongozo wa namna ya
kuwafundisha wanafunzi.

Amesema hali ya
ufaulu kwa wanafunzi nchini hairidhishi na kwamba uwepo wa vitabu hivyo
utasaidia pakubwa kuinua sekta ya elimu nchini.
“mwaka jana wanafunzi
16000 wa darasa la nne walifeli na 4000 hawakufanya mitihani kwa sababu
tofauti, hii si hali nzuri hata kidgo” alisema Rijali.
Rijali amesema
kutokana na haja kubwa ya uwepo wa vitabu hivyo nchini kila siku alikua
akiandamwa na wadau kwa maswali ya kutaka kujua vitabu hivyo ni lini
vitakuja nchini, amesema hivi sasa ameshapata jibu muwafaka huku akisema
kua mambo katika sekta ya elimu yanaelekea pazuri hususan katika lugha
ya kiingereza.
Awali akimkaribisha
Bi Safia Mkuu wa Programu kutoka Milele Zanzibar Foundation Bi Khadija A
Sharif amesema kua lengo la kuleta vitabu hivyo ni kutaka kukuza
uwelewa wa wanafunzi katika lugha ya kiingereza.
Bi Khadija amewataka
walimu waliyohudhuria katika mkutano huo kua makini na miongozo
waliyopatiwa ili kuwafundisha wanafunzi wao kiufasaha zaidi hatimae
lengo lifikiwe.
Mratib wa kituo cha
elimu Wingwi (TC Coordinator) mwalimu Shoka Hamad Abeid ambae ni
mshiriki katika mafunzo hayo amesema kua, kilichofanywa na taasisi ya
Milele ni ukombozi katika sekta ya elimu kwani kila kitu katika
mafanikio kunahitajika nyenzo na uwepo wa vitabu hivyo ni nyenzo kubwa
itakayowawezesha kufanya vizuri.
Kwa upande wake
mwalimu Rehema Ali Said wa skuli ya Amini Islamic Primary ameonyesha
kufurahishwa sana juu ya utambulisho wa vitabu hivyo huku akisema kua
ana matumaini makubwa ya kufanya vizuri wanafunzi katika lugha ya
kiingereza tofauti na hali ilivyokua.
Amefahamisha kua,
vitabu hivyo ni tofauti na vya awali kwakua hivi vya sasa kiurahisi
zaidi vitamuwezesha mwanafunzi kuweza kutamka maneno ya kiingereza kwa
wepesi na kwa kasi zaidi hali ambayo itapelekea uchapu katika
kuzungumza.
Katika mafunzo hayo
walimu wamepatiwa mbinu mbalimbali zitakazo mfanya mwanafunzi kufahamu
kwa kwaharaka kupitia michoro na maelezo elekezi yaliyomo katika vitabu
hivyo vinavyotakiwa kutumika kuanzia sasa katika skuli zote za unguja na
pemba.

chanzo: zanzibar24.
Comments