Wakizungumza
juzi kuhusiana na tatizo hilo, wafugaji hao walidai kuwa ukame uliozikumba
sehemu mbalimbali wilayani humo umesababisha mifugo yao ikiwamo ng’ombe, mbuzi
na punda kufa.
Alex Mollel
mmoja kati ya wafugaji hao alisema yeye binafsi amepoteza zaidi ya ng’ombe 250
kutokana na ukame na wafugaji wengi pia wamepata hasara kutokana na ukame huo ambao
haujawahi kutokea.
“Huu ukame wa
kipindi hiki umetusababishia hata bwawa la Kidawashi kukauka na pia
mifugo imekosa maji na malisho hali inayosababisha hasara kubwa kwa wafugaji
wengi,” alisema Mollel.
Alice Laizer alisema
wingi wa mifugo umesaidia wafugaji wengine kubaki na baadhi ya mifugo baada ya
mingine kufa, kwani endapo wangekuwa na mifugo michache, wengi wao wangeishiwa
mifugo yote.
“Mfano kina
Orenji walikuwa na ng’ombe 2,500 na hao 500 wakafa hivyo wamebaki ngombe 2,000
na baada ya miaka miwili au mitatu hiyo iliyobaki itazaana na kurudia idadi ya
awali,” alisema Laizer.
chanzo:Mwananchi.
Comments