Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM, Humphrey Polepole alisema katika taarifa yake aliyoituma kwa vyombo vya habari kuhusu ziara hiyo.
Alisema ujumbe huo wa wanachama wa Chama cha Kikomunisti cha China, unatarajia kufika nchini leo na kuwa na ziara ya kikazi kwa siku nne.
“Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinapenda kuwafahamisha wanachama wake na umma wa watanzania kwamba siku ya Jumanne (leo) tarehe 21 Machi 2017 kitapokea ujumbe wa viongozi na maofisa kutoka Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) ambao watakuwa hapa nchi kwa ziara ya kikazi ya siku nne,” alisema Polepole.
Wengine watakaoongozana na meya huyo ni Mjumbe wa Kamati ya Msingi ya CPC (Politi-bureau), Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha CPC na Katibu wa Kamati ya CPC ya Manispaa ya Jiji Ia Beijing.
Pia alisema Jinlong ameambatana na viongozi wengine wawili ambao ni Xu Luping, Makamu wa Waziri wa Idara ya Kimataifa ya Kamati Kuu ya CPC na Zhang Yankun Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Kamati ya CPC ya Manispaa ya Jiji la Beijing.
“Ifahamike kwamba Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Chama cha Kikomunisti cha China wamekuwa na urafiki wa muda mrefu tangu kipindi cha Uhuru, ukombozi wa kusini mwa Afrika hadi sasa. Chama Cha CPC kitatumia ziara hiikujifunza na kubadilisha uzoefu na CCM,” alisema.
Katika hatua nyingine, alisema ujumbe huo pia utamtembelea Mwenyekiti wa CCM ambaye ni Rais wa Awamu ya Tano, John Magufuli na Makamu wa Mwenyekiti wa CCM Tanzania Zanzibar ambaye ni Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Ali Mohamed Shein.
chanzo:Habarileo.
Comments