Mazrui awataka wananchama wa CUF kupuuza uamuzi wa Lipumba.

Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (Cuf) Zanzibar, Nassor Ahmed Mazrui, alimshangaa Mwenyekiti wa chama hicho, Profesa Ibrahimu Lipumba kwa hatua yake ya kuwavua uongozi wakurugenzi sita wa chama hicho wanaofanya kazi zao Zanzibar jambo ambalo ni kinyume na katiba ya CUF.
Ameyazungumza hayo jana kwenye ofisi za chama hicho zilizopo Vuga mjini  Zanzibar,
Mazrui alisema katiba ya chama chao haimpi mwenyekiti uwezo wa kuwavua uongozi hivyo aliwataka wanachama wa Cuf kupuuza uamuzi huo.
Aidha alisema, Profesa Lipumba  anafahamu kuwa hana uwezo wowote ndani ya chama hicho kisheria,hivi sasa licha ya kuwa  bali lengo lake ni kuhakikisha anakihujumu Chama kwa kutumia mbinu mbalimbali kwa maslahi binafsi.
Alisema katika Katiba ya Cuf  Ibara ya 9(i) na (f), inaeleza kuwa mwenyekiti ana uwezo wa kuteua nafasi mbalimbali kama wakurugenzi, manaibu wao na viongozi wengine, lakini haimpi uwezo wa kumvua uongozi kiongozi aliyemteua bila ya idhini kutoka kwa kamati ya utendaji ya chama na kuridhiwa na wajumbe wa Baraza Kuu.
Mkurugenzi wa Habari, Uenezi na Mawasiliano ya Umma wa Cuf, Salum Biman alisema anachokifanya Profesa Lipumba amekua anashangaza sana watu licha ya kuwa anafahamu si kiongozi ni  mwanachama wa Cuf.
chanzo:zanzibar24.

Comments