Maseneta Marekani: Majengo ya Trump hayakupelelezwa na Obama.

Moja ya majengo yanayomilikiwa na Rais TrumpViongozi wa kamati ya maseneta wa Republican na Democratic Richard Burr na Mark Warner wamesema hakuna dalili yoyote inayoonyesha kuwa majengo ya Trump yalikuwa yakifuatiliwa kabla na baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka jana.
Mwenyekiti wa tume ya uchunguzi amesema pia hakuamini madai hayo yaliyotolewa na Rais Trump dhidi ya mtangulizi wake Barack Obama.

Katibu wa Rais Trump Sean Spicer amesema uchunguzi haujafanyika vya kutosha juu ya suala hilo.
Awali Trump alimtuhumu Obama kuwa anamfanyia upeleleziHakuweka wazi kuwa ni taarifa za aina gani ambazo bado hazijawekwa wazi.
chanzo:Bbc.

Comments