Masauni alisema jeshi hilo ili lifanikiwe katika mapambano yake na
wahalifu , nguvu ya wananchi inahitajika sana katika utoaji wa taarifa
ya matukio hayo.
Akizungumza na mamia ya wananchi wa Kijiji cha Bungu wilayani Kibiti,
Masauni alisema jeshi hilo limejipanga kikamilifu kwa kupambana na
wahalifu na litahakikisha wahalifu hao wanakamatwa wote ili wakazi wa
maeneo hayo kuendelea kufanya shughuli zao za kuijenga nchi kama kawaida
bila wasiwasi wowote. Hata hivyo aliwahakikishia usalama wananchi
waendapo watatoa ushirikiano kwa jeshi hilo.
“… ili amani hii iweze kudumu, mnatakiwa kutoa ushirikiano kwa Jeshi
la Polisi pale ambapo mnakuwa na taarifa na wasiwasi na mtu yeyote
katika maeneo yenu ambaye hana nia nzuri na usalama wenu,” alisema
Masauni.
Alisema Jeshi la Polisi halipaswi kuogopwa na raia mwema, ni rafiki
kwa kila Mtanzania mwema ambaye ana uzalendo wa dhati na nchi yake,
jeshi ni rafiki ya wananchi, hivyo wananchi wanapaswa kuwa karibu na
Jeshi kwa kuwa hao ndio walinzi wa wananchi pamoja na mali zao.
chanzo:Habarileo.
Comments