
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es
Salaam Jumanne hii maadhimisho hayo yataongozwa na maandamano ya
Wanawake na wadau mbalimbali, na yataanzia katika Shule ya Msingi
Mabatini kuelekea viwanja vya Mwembeyanga.
Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani Mwaka huu yanaongozwa na
kauli mbiu isemayo “Tanzania ya viwanda, Wanawake ndio Msingi wa
Mabadiliko ya Kiuchumi”.
Kauli mbiu hiyo inalenga kuikumbusha jamii kuhusu umuhimu wa kujenga
mazingira wezeshi kwa Wanawake hasa kutambua mchango wao katika kuleta
Maendeleo yao na ya jamii kwa ujumla.
Taarifa hiyo pia imeikumbusha jamii kuhusu wajibu wake ikiwa ni
pamoja na kuwashirikisha, kuwaamini na kuwapa Wanawake haki sawa katika
nafasi za Elimu, Uchumi na uongozi ili wawe chachu ya mabadiliko yenye
lengo la kuifanya Tanzania kuwa nchi ya viwanda.
Maadhimisho hayo yataambatana na maonesho ya kazi za ujasiriamali
yanayoendelea katika uwanja wa Mwembeyanga, ambapo Asasi za kiraia na
vikundi mbalimbali vya wanawake vitaonesha bidhaa zao.
chanzo: zanzibar24.
Comments