“Vita ya dawa za kulevya ni kubwa, hata hivyo Serikali tunaendelea
kupambana nayo. Nchi ilikuwa inapoteza vijana ambao walikuwa
wamejiingiza katika biashara haramu ya dawa za kulevya.
Nawaomba
msithubutu kuingia huko mtafungwa,” amesema.
Kwa mujibu wa taarifa ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa vyombo vya habari,
Waziri Mkuu Majaliwa ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na Umoja wa
Watanzania wanaoishi nchini Mauritius katika mkutano alioutisha kwenye
Hoteli ya Meridien mjini Port Louis.
Alisema katika kudhibiti biashara hiyo haramu ya dawa za kulevya,
serikali iliamua kuunda Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Dawa za
Kulevya (DCEA) na inafanya kazi vizuri.
“Na tutakamata kila mtu anayejihusisha na biashara hiyo bila kujali cheo, uwezo na mamlaka aliyonayo,” aliongeza.
Alisema mamlaka hiyo inafanya kazi ya kutafuta wazalishaji, watumiaji
na wafanyabiashara, lengo likiwa ni kuokoa vijana ambao wameshindwa
kutimiza ndoto zao kutokana na madhara waliyoyapata baada ya kutumia
dawa za kulevya.
Aidha, amewataka Watanzania hao walioko Mauritius kujenga mshikamano wa pamoja na wawe na uzalendo na nchi yao.
Pia wawe mabalozi wazuri wa kutangaza vivutio vya Taifa. Alisema ni
vema wakatumia fursa walizonazo katika kutafuta wawekezaji na
kuwashawishi waje nchini na kuwekeza kwenye sekta mbalimbali zikiwemo za
viwanda, uvuvi, nishati na utalii.
Kwa upande wake, Waziri wa Fedha na Mipango wa Serikali ya Mapinduzi
Zanzibar, Dk Khalid Salum Mohammed amewaomba Watanzania hao wazidishe
mshikamano miongoni mwao kwa kuwa umoja wao ndio nguzo yao.
Naye Mwenyekiti wa muda wa Umoja wa Watanzania waishio Mauritius,
Donald Kongwa ambaye ni Ofisa wa Benki ya Standard Chartered nchini
Mauritius, amemhakikishia Waziri Mkuu kwamba kipato wanachokipata
watakitumia kwa kuwekeza Tanzania kwa lengo la kukuza uchumi wa Taifa.
chanzo:Habarileo.
Comments