Mahakama hiyo ya kikatiba imesema kuwa bi Park alikiuka sheria na kuharibu demokrasia.
Park ambaye ndio mwanamke wa kwanza kuwa rais nchini humo alihusishwa na kashfa ya kujipatia fedha kwa njia za ufisadi kutoka makampuni makubwa nchini humo na rafikiye mkubwa Choi Soon-Sil.
Bi Park huenda akakabiliwa na mashataka ya uhalifu.
Lakini wafuasi wake pia walionekana na kumekuwa na mzozano kati ya makundi hayo mawili.
Uchaguzi wa urais sasa utafanyika katika kipindi cha siku 60.
Rais huyo sasa amepokonywa uwezo wa kutoshtakiwa na sasa anaweza kusimamishwa kizimbani na kufunguliwa mashtaka.
Bi Park alikuwa amesimamishwa kuhudumu kama rais tangu mwezi Disemba huku waziri mkuu wa taifa hilo akichukua majukumu ya kuongoza taifa.
Bi Choi wakati huohuo ameshtakiwa kwa kuchukua hongo kwa madai ya kuyashinikiza makampuni makubwa kumpa pesa huku akiahidi kwamba kampuni hizo zitapendelewa na serikali.
Bi Park ameshtumiwa kwa kushirikiana na Choi.
Jopo la majaji wanane katika mahakama ya kikatiba liliangazia mashtaka yanayomkabili bi Park na kuamua kwamba kulikuwa na sababu mwafaka za kumwachisha kazi.
Makundi ya watu yalikuwa yemekongamana nje ya jengo la mahakama hiyo kusikiza uamuzi utakaotolewa swala ambalo limezua maandamano katika mji mkuu wa Seoul na miji mingine.
chanzo:Bbc.
Comments