Maelfu wahamishwa kufuatia mlipuko kwenye ghala la silaha Ukrain.

Maelfu wahamishwa baada ya mlipuko kwenye ghala la silaha UkrainKaribu watu 20,000 wanahamishwa kufuatia kutokea misururu ya milipuko kwenye ghala kubwa la kuhifadhi silaha mashariki mwa Ukrain, kisa ambacho kimetajwa na maafisa kuwa cha kuhujumu.

Ghala hilo lililo eneo la Balakliya liko umbali wa karibu kilomita 100 kutoka eneo la mapigano na waasi wanounga mkono Urusi.


Hutumika kuhifadhi maelfu ya tani ya risasi na makombora.

Makundi ya uokoaji yanaongoza shughuli kubwa ya kuwahamisha watu wanaoishi mji huo na vijiji vilivyo karibu.

Maelfu wahamishwa baada ya mlipuko kwenye ghala la silaha UkrainEneo lote la ghala hilo lina ukubwa wa karibu ekari 350.

Silaha kutoka ghala hilo hutumiwa na vikosi vilivyo eneo la mzozo katika maeno yaliyo karibu ya Luhanks na Donetsk.

Mamlaka inachunguza njia tofauti milipuko hiyo ilisababishwa. waziri wa ulinzi Stepan Poltorak alisema kuwa kuna uwezekano wa kifaa cha kulipuka kuangushwa na ndege isiyokuwa na rubani.

Ndege isiyokuwa na rubani inaripotiwa kutumika kujaribu kuwasha moto ghala hilo mwezi Disemba mwana 2015.

Maelfu wahamishwa baada ya mlipuko kwenye ghala la silaha UkrainZaidi ya watu 9,700 wameuawa kwenye mzozo ambao ulilipuka mwaka 2014 wakati Urusi ilimega rasi ya Crimea.
 chanzo:Bbc.

Comments