
Akizungumza na Waandishi wa habari amesema migogoro yote kwenye chama hicho imesababishwa na Lipumba akiwa na lengo la kukivuruga chama kwa makusudi na kudai kuwa ametumwa na vyama vya upinzani.
Hata hivyo amesema chama cha CUF kimefanyiwa hujuma mbalimbali ili kivunjike moyo katika majukumu yake ya kutaka kuchukua dola ili kuwapa wazanzibar haki zao na kuahidi kuwa mabadiliko yatakuja Zanzibar baada siku chache zijazo.
chanzo:Zanzibar24
Comments