Mfumo huo mpya wa aina ya IVF utatumika kuwalinda watoto kutofariki kutokana na magonjwa yanayosambazwa kupitia jeni.
Kundi hilo katika kituo cha rutba za uzazi cha Newcastle kimesema kuwa ni habari njema kwa wagonjwa.
Na sasa kituo hicho sasa kinatarajia mtoto wa kwanza kuzaliwa 2018 ikiwa ndio mapema.
Mfumo huo unalenga kukabiliana na magonjwa ya jeni ambayo huwawacha watu kukosa nguvu za moyo wao kufanya kazi.
Baadhi ya watu wamepoteza watoto kadhaa kwa sababu ya ugonjwa huo.
Ugonjwa
huo husambazwa kutoka kwa mama, kwa hivyo mbinu ya kutumia yai
lililofadhiliwa, na yai la mama pamoja na mbegu za kiume za baba
imeimarishwa.
Mtoto anayepatikana huwa na vinasaba vya jeni
kutoka kwa mfadhili, lakini mfumo huo sasa ni wa haki na sasa unafuata
maadili na uko tayari kufanyakazi kisayansi.
chanzo:Bbc.
Comments