Katika serikali hiyo mpya, mbali na chama cha 'Uadilifu na Ustawi' ambacho kina viti vingi bungeni, kikiwa kinahodhi jumla ya viti 125 kati ya 395 vya bunge, mawaziri watatoka pia kutoka vyama vya National Rally of Independents (NRI), Socialist Union of Popular Forces (USFP), Popular Movement (MP), Party of Progress and Socialism (PPS), na Constitutional Union (UC).
Aidha Waziri Mkuu wa Morocco amesisitiza kuwa, hadi sasa bado mazungumzo yanaendelea na vyama hivyo kwa ajili ya kugawana wizara.
Licha ya kupita miezi kadhaa tangu ulipofanyika uchaguzi wa bunge nchini humo, mazungumzo yaliyofanyika hadi sasa kwa ajili ya kuunda serikali, hayajawa na tija tarajiwa.
Kwa mujibu wa mfumo wa uchaguzi nchini Morocco, hakuna chama kinachoweza kupata ushindi mutlaki na hii ikiwa na maana kwamba, washindi wanatakiwa kuingia katika mazungumzo kwa ajili ya kuunda serikali ya mseto, suala ambalo huwa linapunguza ushawishi wa kisiasa wa vyama nchini humo.
Aidha Waziri Mkuu wa Morocco amesisitiza kuwa, hadi sasa bado mazungumzo yanaendelea na vyama hivyo kwa ajili ya kugawana wizara. Licha ya kupita miezi kadhaa tangu ulipofanyika uchaguzi wa bunge nchini humo, mazungumzo yaliyofanyika hadi sasa kwa ajili ya kuunda serikali, hayajawa na tija tarajiwa.
Hata hivyo mfalme wa Morocco anasimamia baraza la vyombo vya mahakama, idara ya usalama na baraza la mawaziri. Kadhalika baadhi ya nyadhifa muhimu kama vile Wizara ya Mambo ya Ndani pia ziko chini ya mfalme.
Katika uchaguzi wa bunge uliofanyika mwanzoni mwa mwezi Oktoba mwaka jana na ulioshuhudia ushiriki mkubwa wa wananchi, chama chenye mielekeo ya Kiislamu cha 'Uadilifu na Ustawi' kiliweza kupata akthari ya viti vingi bungeni.
Awali Abdelilah Benkirane, waziri mkuu wa zamani, alikuwa ameahidi kuwa, endapo chama chake kitaibuka na ushindi katika uchaguzi huo, angefanya marekebisho ya kiuchumi nchini, sambamba na kuzifanyia mabadiliko sheria kadhaa za ndani kwa minajili ya kutatua matatizo mengi ya wananchi.
Mwanzoni mwa harakati zake Saadeddine Othmani alitangaza kuwa angeunda serikali hiyo ndani ya kipindi kisichozidi siku 15. Inafaa kuashiria kuwa uundaji wa serikali nchini Morocco, unahitaji chama husika kupata viti 198 katika bunge la wawakilishi.
Tayari vyama sita ambavyo vina jumla ya viti 240 vimekubaliana kuunda serikali ya mseto nchini humo.
Hii ni katika hali ambayo, hatua ya ucheleweshaji kuundwa serikali mpya, ilipelekea kuibuka migogoro ya kisiasa kati ya mirengo tofauti ya kisiasa nchini, katika hali ambayo taifa hilo bado linakabiliwa na migogoro mingine ya kiuchumi na kijamii.
Kabla ya hapo Mfalme Mohammed wa VI alitangaza kuwa, matatizo yanayozikabili nchi za Afrika, ikiwemo umasikini, kubaki nyuma kimaendeleo, uhajiri na ugaidi, vinatokana na siasa mbovu za ukoloni ulioshuhudiwa katika nchi za bara hilo.
Morocco inakabiliwa na matatizo mbalimbali ikiwemo, ukosefu wa ajira kwa vijana, kuongezeka kiwango cha madeni ya ndani na nje, ongezeko la upinzani wa ndani na kadhalika tishio la ugaidi.
chanzo:parstoday.
Comments