Akizungumza
leo Oleleshwa alisema ameamua kwa hiyari yake kuachia nafasi hiyo
aliyoishikilia kwa zaidi ya miaka minne sasa kwa dhamira safi na moyo mweupe,
hivyo anampisha katibu mwingine.
Amesema
alijiunga na Chadema Mei, 2012 akiwa anasoma chuo cha wanyamapori Mwika mkoani
Kilimanjaro na kisha akaanza harakati za kukijenga chama hicho jimbo la
Simanjiro.
Alisema japo
wapo watakaobeza jitihada na juhudi zake, lakini ameshiriki kufanikisha
ushindi wa Chadema kwa kupata mbunge, madiwaniwa kata sita na baadhi ya wenyeviti wa vijiji na vitongoji.
Alisema
kujiuzulu kwake haina maana kuwa ameenda likizo ya kutofanya kazi ya Chadema
jimbo la Simanjiro, kwani bado ana wajibu kama mwanachama kwa kuilinda,
kuitetea na kuijenga.
chanzo:mwananchi.
Comments