JPM azungumza na Dk Shein, amtakia heri ya ‘birthday.

Rais John Pombe Magufuli leo amekutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Ali Mohamed Shein, Ikulu ya Chamwino mjini Dodoma.



Katika taarifa iliyotolewa  kwa vyombo vya habari na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Ikulu, Rais Magufuli amesema wamezungumza mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na kumtakia heri  ya siku ya kuzaliwa Dk.




Kwa upande wake Rais Dkt. Ali Mohamed Shein amesema anamshukuru Rais Dkt.Magufuli kwa kumtakia heri katika siku yake muhimu ya kuzaliwa na hivyo wamekutana kubadilishana mawazo katika kuhakikisha wanajenga nchi na kusonga mbele.



''Siku ya kuzaliwa ni siku ya furaha lazima ikumbukwe lazima isherehekewe, mimi siku yangu ya kuzaliwa sisherehekei sana lakini huwa nafurahi sana  na leo nimefurahi sana'' amesema Dkt. Shein.



Shein amesema ametumia siku yake ya kuzaliwa kumtembelea Rais Dkt.Magufuli ili waweze kubadulishana mawazo kwani wana kazi kubwa ya kujenga nchi.


chanzo:Mwananchi.

Comments