Jeshi la Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi lakamata Viroba na Dawa za kulevya.

Jeshi la polisi limefanikwa kukamata kiasi kikubwa cha pombe iliopigwa marufuku aina ya viroba katika mtaa wa mkunazini iliyokuwa inauzwa kwa kificho na Bw. Mandai Halfani Mandaria pamoja na kiasi kikubwa cha bangi katika nyumba ya Mpenda Majaliwa Khamis wa kizimbani wilaya ya magharibi unguja na kete elfu moja mia mbili za dawa kulenya aina ya Heroin.


Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari kamanda wa polisi mkoa wa Mjini Magharibi Kamishna Msaidizi Mwandamizi Hassan Nassir Ali amesema jeshi la polisi limejipanga kumaliza uingizaji, usambazaji na matumizi ya dawa za kulevya katika Mkoa wa mjini magharibi kabla kumalizika mwaka 2017.

Kamanda Nassir amesema jeshi hilo limejipanga kikamilifu kuhakikisha linamaliza tatizo hilo haraka iwezekanavyo na kuwaomba wananchi wa mkoa huo kuunga mkono juhudi za jeshi la polisi katika kufikia malengo waliyojiwekea.

 chanzo:zanzibar24.

Comments