Neil Gorsuch ameambia kikao cha bunge la Seneti kwamba hakuna mtu
yeyote aliyemtaka kutoa ahadi kuhusu jinsi atakavyofanya maamuzi yake
pindi atakapoidhinishwa kuwa jaji katika mahakama hiyo.
Amesema
angekataa uteuzi huo iwapo Bw Trump angemtaka kubatilisha uamuzi wa
kihistoria wa mahakama katika kesi Roe v Wade ambao ulihalalisha utoaji
wa mimba.
Bw Gorsuch pia alishutumu vikali hatua ya Trump
kuwashambulia kwa maneno majaji wa mahakama mara kwa mara na kusema
"inavunja moyo".
Februari, rais huyo alimweleza jaji
aliyebatilisha marufuku yake ya usafiri dhidi ya raia wa nchi saba kama
"mtu huyo anayeitwa jaji".
Bw Gorsuch faraghani aliwaambia maseneta kwamba hilo lilikuwa na
maana kwamba iwapo kungetokea shambulio la kigaidi katika ardhi ya
Marekani, basi jaji huyo ndiye angekuwa lawamani.
"Mtu yeyote
anapokosoa uaminifu na maadili au nia ya jaji wa mahakama, hilo
linavunja moyo.
Nafikiri linatamausha - kwa sababu naujua ukweli,"
alisema.
Alipoulizwa iwapo hilo linamhusu pia rais, alijibu: "Mtu yeyote ni mtu yeyote."
Msemaji
wa ikulu ya White House Sean Spicer baadaye aliandika kwenye Twitjer
kwamba Bw Gorsuch alikuwa akizungumza "kwa mapana" na kwamba hakumtaja
mtu kwa jina."
Wakati wa kikao chake cha kwanza kuhojiwa na
maseneta, Gorsuch, ambaye ni jaji wa Colorado aliulizwa maswali mengi
kuhusu msimamo wake.
Maseneta wa Democrat walisisitiza kuhusu
baadhi ya mambo yenye utata, lakini alisisitiza mara kwa mara kwamba
ingekuwa makosa kwake kueleza angetoa uamuzi wa aina gani katika kesi
yoyote hilo.
Alisema huo ungekuwa ndio "mwanzo wa mwisho" wa mahakama huru.
Bw Gorsuch, amependekezwa kujaza nafasi iliyoachwa wazi kutokana na kifo cha Jaji Antonin Scalia miezi 13 iliyopita.
chanzo:Bbc.
Comments