Zaidi ya wakimbizi 30 kutoka Somalia walioko Yemen wameuawa katika
shambulio lililolenga boti waliokuwa wakisafiria wakiwa kwenye bahari
ya Shamu.
Vikosi vinavyoshughulikia doria za baharini katika
bandari ya Hodeidah inayodhibitiwa na waasi Wa-houthi vinasema boti
hilo lilikuwa linatoka Yemen kuelekea Sudan wakati liliposhambuliwa kwa
kombora.
Kituo cha habari kinachomilikiwa na waasi hao kimedai shambulio hilo limefanywa na ndege ya hlikopta aina ya Apache .
Zaidi ya majeruhi 80 wa mkasa huo wamekimbizwa hosptialini.
Eneo
la Hodeidah ni mojawapo linalokumbwa na mashambulio ya mara kwa mara
kutokana na mzozo wa kivita unaoendelea baina ya jeshi la Yemen
linaloungwa mkono na lile la Saudia, dhidi ya waasi hao wa Houthi
wanaopinga serikali ya Yemen.
chanzo:Bbc.
Comments