Gwajima Ajitosa Sakata La Vanessa Mdee......Ahoji Sababu za Bashite Kutoroka na Kukimbilia Afrika Kusini.
#FreeVanessaMdee
haijaishia kutrend kwenye midomo ya mashabiki na wasanii pamoja na
kwenye mitandao ya kijamii peke yake, weekend hii.
Vee
Money ameonekana kuwa special katika mastaa wote waliohusishwa na
skendo ya madawa ya kulevya baada ya umma kuonesha kumtetea kwa nguvu
zote.
Muimbaji
huyo pia amepata baraka toka kwa Mchungaji Gwajima ambaye tangu naye
ahusishwe na biashara hiyo amekuwa akifurumisha mabomu dhidi ya mkuu wa
mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.
Akizungumza mbele ya waumini wa kanisa lake, Gwajima alisema:
"Sasa
hapo ndio najiuliza, polisi na uhamiaji waseme kwanini wanasuasua na
kuna makosa niliyoyataja angalau saba ya jinai wakati wengine wamelala
ndani kwa kuhisiwa tu wakiwemo wanamuziki kwa mfano Vanessa Mdee.
"Amelala
ndani tu alikuwa nje wakati sisi ametajwa naye ametajwa amerudi ndani
leo siku ya tatu Vanessa Mdee leo yuko ndani kwa kuhisiwa tu.
"Lakini
huyu mpaka tumetaja Daudi Bashite yupo katorokaje? Huyu kakimbiaje?
Vanessa Mdee simfahamu wala simjui lakini alikuwa ana performing zake
nje ya nchi kashikwa pale yuko ndani leo, huyu katorokaje? Kwanini
wengine wako ndani na wengine wanazunguka mitaa ya South Africa wakati
walitakiwa wawe hapa na wao, mbona mimi nilienda kulala tu?"
chanzo:Mpekuziblog.
Comments