
Mbowe ameyasema kufuatia tuhuma nyingi zilizoibuka hivi karibuni
kuhusu kiongozi huyo.
Miongoni mwa tuhuma hizo ni kuhusu uhalali wa
vyeti vya Makonda, uongozi wake usiofuata sheria za utawala bora,
matumizi mabaya ya mali za serikali, utajiri usio na majibu pamoja na
kuingilia uhuru wa vyombo vya habari.
Baadhi ya viongozi na wadau wengine pia wamelizungumzia suala hili
kuwa siyo la kufumbiwa macho huku wakimtaka Rais Dkt John Pombe Magufuli
kumchukulia hatua kiongozi huyo.
Miongoni wa viongozi waliotoa maoni
yao ni pamoja na Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Tundu
Lissu ambapo amemtaka Rais Dkt Magufuli kutengua uteuzi wa Makonda.
Licha ya tuhuma zote hizo kutolewa na vyombo vya habari pamoja kwenye
mitandao ya kijamii, Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda
hajasema lolote kuhusiana hayo yanayozungumzwa, Sekretarieti ya Maadili
ya Viongozi wa Umma haijazungumza wala Baraza la Mitihani la Tanzania.
chanzo: zanzibar24.
Comments