
Akizungumza nje
ya ukumbi wa mikutano wa Benjamin Mkapa kilipofanyika kikao hicho, Mwangonela
alisema tangu ashinde rufaa Desemba 17 mwaka jana hajawahi kupewa au kuambiwa
kwamba amekatiwa rufaa na kwamba, kuibuka kwa hoja hiyo katika kikao hicho ni
mwendelezo wa fitina za kisiasa.
Diwani huyo
alihukumiwa kifungo cha miaka mitatu jela mwaka 2015 baada ya kutiwa hatiani na
Mahakama ya Hakimu Mkazi Mbeya, Novemba 17, 2015 kwa kosa la kuvunja ghala na
kuiba magunia 171 ya ngano mali ya Chuo cha Utafiti na Kilimo Uyole.
Hata hivyo,
alikata rufaa Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya na alishinda Desemba mwaka jana baada
ya Jaji Mfawidhi wa mahakama hiyo, Noel Chocha kuamuru arejeshwe udiwani wake.
Mwanasheria wa
Jiji la Mbeya, Davis Mbembela alisema diwani Mwangonela asingeweza kuapishwa
kwa kuwa baada ya kushinda, Jamhuri ilikata rufaa hivyo bado anakabiliwa na
kesi.
chanzo;Mwananchi.
Comments