Walaji wa nyama
ya nguruwe ‘kitimoto’ wilayani Kalambo mkoani Rukwa watakikosa kitoweo hicho
kwa muda usiojulikana baada ya Serikali kupiga marufuku watu kula nyama hiyo.
Hatua hiyo
imefikiwa baada ya nguruwe 150 kufa kwa ugonjwa wa mafua wa African Swine Fever
na kuwaacha wengine wakiwa hoi.
Mkuu wa Wilaya
ya Kalambo mkoani Rukwa, Julieth Binyura alisema ugonjwa huo ulijitokeza miezi
mitatu iliyopita kwenye Kitongoji cha Masazi na kusambaa
katika kata za Legezamwendo na Mambwe Nkoswe.
Ofisa Mifugo wa
Wilaya ya Kalambo, Wilbroad Kansapa alisema nguruwe wote wanaozagaa
mitaani watakamatwa na mizoga yote ifukiwe.
chanzo:Mwananchi.
Comments