imekanusha uvumi unaosambazwa kwenye mitandao ya kijamii kuhusu uuzaji wa viwanja katika eneo la Mkonze lililopo mkoani Dodoma.
Tamko hilo
limetolewa hivi karibuni mkoani Dodoma na Kaimu Meneja Uhusiano wa CDA, Angela
Msimbira kutokana na kusambaa kwa ujumbe huo katika mitandao mbalimbali ya
kijamii.
Angela amesema
taarifa hizo ambazo hazieleweki zimekuwa zikidai kuwa viwanja hivyo ni halali
na ukinunua unapewa hati na CDA ambayo ndiyo imepewa dhamana ya ugawaji wa
viwanja mkoani humo.
“Mamlaka yetu
inapenda kuutarifu umma kuwa taarifa hizo si za kweli hivyo wananchi wanatakiwa
kuzipuuza na kuendelea kufata utaratibu kwani mamlaka hiyo ina utaratibu
uliopangwa wa namna ya kupata viwanja vilivyo halali,”amesema Angela.
chanzo:mwananchi.
Comments