Akizungumza katika mkutano wa mashauriano kati ya Bodi ya Usajili wa
Wabunifu Majengo, Wakadiriaji Ujenzi pamoja na Jeshi la Polisi, Dk
Ambwene alisema Sheria Namba 4 ya Mwaka 2010, inaitaka bodi yao iwe
inasajili na kuratibu mienendo ya wabunifu majengo.
Alisema bodi yao imepanga kukagua miradi 1,800 ya ujenzi nchi nzima
mwaka huu, baada ya mwaka jana kukagua miradi 1,227 na kwamba,
watachukua hatua mbalimbali kwa miradi iliyokiuka sheria, ikiwa ni
pamoja na kusimamisha shughuli za ujenzi.
“Bodi ina jukumu la kuingia na kukagua miradi ya ujenzi ili
kuhakikisha imebuniwa na inasimamiwa na wataalamu waliosajiliwa. Hadi
sasa Bodi yetu imesajili watalamu 1,442 na makampuni 393,” alisema.
Alimwomba Kamishna wa Operesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi, Nsato
Marijani aendelee kuwahimiza wataalamu wa ujenzi waliosajiliwa
kuhudhuria mafunzo mbalimbali yanayoandaliwa na bodi hiyo.
Kwa upande wake, Kamishna Marijani aliipongeza AQRB kwa juhudi za ukaguzi wa maeneo ya ujenzi katika mikoa yote nchini.
Alisema Jeshi la Polisi nchini litaendelea kusimamia sheria hiyo na
ameiomba AQRB kuhakikisha wanatoa ushirikiano kwa polisi pale
wanapohitajika.
chanzo:Habarileo.
Comments