Matokeo ya
utafiti uliofanywa na shirika la Twaweza Februari yanaonyesha kuwa asilimia 51
ya kaya hazikuwa na Chakula chankutosha au mwanakaya ameshinda njaa kwa sababu
hakuweza kupata Chakula.
Akifafanua
kuhusu utafiti huo leo Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Twaweza, Aidan Eyakuze
alisema takwimu zake zimekusanywa kutoka kwa wahojiwa 1,800 wa Tanzania Bars
kati ya Septemba 14-26, 2016 nabkutoka kwa wahojiwa 1,610 kati ya February
9-15, 2017.
"Kwa mujibu
wa wananchi wengi, Uhakika wa kupata chakula umepungua kati ya Septemba 2016 na
February 2017.
Asilimia 65 ya wananchi walikuwa na hofu ya
Maya zaobkukosa chakula cha kutosha ikilinganishwa na asilimia 45 waliosema
hiyo Septemba 2016," alisema Eyakuze.
"February
2017 asilimia 51 ya wananchi waliripoti kwamba kuna wakati hawakuwa na Chakula
ch kutosha kwa ajili ya kaya zao katika kipindi cha miezi mitatu
iliyopita," aliongeza.
chanzo:Mwananchi.
Comments