
hukumu hiyo iliyotolewa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Wilayani Nzega mkoani Tabora,
imetoa hukumu hiyo baada kugundulika kuwa mtu huyo amembaka mjukuuu wake na kumjeruhi vibaya sehemu zake za siri.
Awali Mwendesha Mashtaka wa Jeshi la Polisi, Melito Ukongoji, aliieleza mahakama hiyo kuwa mtuhumiwa alitenda kosa la kumbaka mtoto huyo Aprili 24 mwaka 2016 baada ya kuachwa na wazazi wake walipokwenda shambani kulima.
Ukongoji alisema, “Baada ya muda wazazi wa mtoto huyo wakiwa shambani walisikia kelele za mtoto na walipokwenda kuangalia nini kimetokea, walikuta tayari mshtakiwa amembaka na kumjeruhi sehemu zake za siri.”
Akisoma hukumu hiyo juzi, Hakimu Mkazi Mfawidhi wa mahakama hiyo, Serafina Nsana, alisema adhabu hiyo imetolewa baada ya mahakama kuridhika na ushahidi uliowasilisishwa na upande wa mashtaka.
chanzo:zanzibar24.
Comments